Mbunge wa jimbo la segerea Mhe Bonnah kaluwa jana aliendelea na ziara yake katika jimbo lake la Segerea kwa kutembelea Kata ya Vingunguti mtaa wa butiama ambapo amejionea kazi inayoendelea ya kufukia bonde la mto msimbazi inayofanywa mwenyekiti wa mtaa huo Elvis bwahama,
Mmomonyoko wa mto huo umeathiri sehemu kubwa Sana ya makaburi ambapo imemlazimu mwenyekiti wa mtaa huo kujaza kifusi eneo la makabuli ili kuyakinga yasiendelee kuondoka na maji
Mh. Bonnah baada ya kujionea hali hiyo ameahidi kutoa mawe kwaajili ya kujenga kingo eneo hilo.
Mbunge aliendelea na ziara yake KATA ya Liwiti ambapo alitembelea barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami kutoka barakuda kwenda chang'ombe.
Matukio mbalimbali katika picha.
Post A Comment: