Viongozi wa ngazi mbalimbali Serikalini , viongozi wastaafu pamoja na mamia ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wameshiriki katika mazishi ya mzee Rashid Mkwachu ambaye ni baba yake mzazi Mke wa Rais mstafu Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete.
Mwili wa mzee Mkwachu umezikwa jana katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mzee Mkwachu alifikwa na umauti Julai 19 mwaka huu na chanzo cha kifo chake kimeelezwa na Msemaji wa familia ya Kikwete,Ridhawani Kikwete kuwa mzee huyo amefariki kutokana na magonjwa ya utu uzima kwani umri wake ulikuwa zaidi ya miaka 100.
Kabla ya mwili kufikishwa makaburi ya Kisuti ibada na dua kumuombea marehemu mzee Mkwachu zilifanyika nyumbani kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete Msasani jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi walioshiriki kwenye maziko hayo ni Rais Mstaafu Al haji Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa.
Akizungumza kwenye msiba huo Sheikh Mkuu wa Tanzania Muft Abuubakary Zubeiry amesema maisha ya binadamu ya kuishi kwenye ulimwengu ni mafupi sana na kwa kawaida ni kati ya miaka 63 na ikitoa zaidi ya hapo ni zawadi tu.
Amesema kuwa viumbe vyote ni vinamuda wake wa kuondoa kwenye huu ulimwengu na hakuna ambaye ataishi milele na kufafanua na kufa si kutoweka moja kwa moja bali ni utaratibu wa maisha ya kutoka kwenye ulimwengu na kwenda akhera.
Kwa upande wake Mjuukuu wa Marehemu Mzee Mkwachu ambaye pia ni Msemaji wa Familia Ridhwan Kikwete alieleza kilichokuwa kikimsumbua babu yake ni magonjwa ya utu uzima.
Ametumia nafasi hiyo kuwashukuru woye ambao wamepata nafasi kwa namna moja a nyingine kuungana nao katiki kipindi hiki ambacho cha majonzi wako.
Post A Comment: