Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan leo ameongoza kikao Cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar katika ukumbi wa mikutano Afisi Kuu CCM Zanzibar.

Kikao hicho kilichobeba ajenda kuu mbili, ambazo ni Mapendekezo ya Kupiga Kura za maoni katika uchaguzi wa Jimbo la Jang’ombe na Mapendekezo ya Wanachama wa CCM wanaomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Uwakilishi jimbo la Jang’ombe.

Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Dkt. Ali Mohammed Shein yupo safarini nje ya nchi hivyo wajumbe walimchagua Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa muda na kuongoza kikao hicho.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: