Mama Kanumba ‘Flora Mtegoa’ amefunguka kuwa kwenye Bongo movies muigizaji anayevaa uhusika vizuri kwa kila Filamu ni Gabo.

Mama Kanumba amesema kila filamu ya Gabo anapoiangalia anaona uhalisia kitu ambacho ni tofauti na waigizaji wengine ambao wanaonekana hawana uhalisia na wanachokifanya.

Mama Kanumba amesema wasanii wote waigizaji wakiwa makini watafika mbali pia watatoka katika giza la kulalamika kuwa filamu hazilipi na kuongeza kwamba kama ingekuwa hazilipi kweli, Gabo angekuwa haendelei kufanya kazi nzuri, ila waigizaji wengi wanajiona wakubwa na kubweteka.

“Msanii ili uwe mkubwa cha kuzingatia inabidi kuwa na heshima kwa watu na kutafuta utofauti ulipo kati yako na wengine, pia kujua vikwazo vinavyokwamisha biashara yako kufikia malengo yako, ukijua hayo basi itakuwa rahisi kwa bidhaa kununuliwa na watumiaji uliowalenga”,

" Naamini akiendelea kusimamia ubora wa kazi zake basi ni rahisi kufika mbali na kuweza kuteka soko la nje ya Nchi, ubora wa kazi zake unajieleza," amesema Mama Kanumba.

Ameongeza kwa kusema wasanii waache kujiona kuwa wamefika kisa wamepata majina na kwamba kila siku wanapaswa wajione wapya na hiyo itawasaidia kufikisha sanaa yao mbali na kutangaza nchi kupitia sanaa yao.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: