Na Hamza Makuza, Mwanza
Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Mbugani Jijini Mwanza kimewataka wananchi kuwapuuza wale wote wanaosema chama hicho kimekuwa kikinunua wanachama kutoka vyama vya upinzania jambo ambalo si sahihi.
Katibu wa Siasa na Uenezi Kata hiyo, Hussein Kim alitoa kauli hiyo jana wakati akimpokea Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbugani ambaye pia ni kada wa Chadema aliyejiunga na CCM baada ya kuguswa na kasi ya utendaji kazi wa chama hicho.
Naye Mwenyekiti huyo wa Mtaa wa Mbugani, Richard Daniel ambaye amejiunga na CCM pamoja na kada mwenzake ambaye pia ni mjumbe wa serikali ya Mtaa wa Mbugani, Zainab Rashid alisema ataendelea kuwatumikia wananchi ingawa kisheria amepotea sifa ya kuendelea kuwa Mwenyekiti baada ya kuhama cha kilichompa udhamini wa kugombea nafasi hiyo
Post A Comment: