WAZIRI Mkuu Kasim Majaliwa anatarajia kuanza ziara yake ya kikazi siku nne Mkoani Kigoma ambapo atatembelea Wilaya nne.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia mstaafu Emanuel  Maganga amesema  ugeni wa Waziri Mkuu ambae ataambatana na Waziri wa Kilimo, Naibu waziri wa madini na Naibu Waziri wa Tamisemi watawasili Mkoani humo Julai 28,2018 saa nne asubuhi.

Alisema ziara hiyo  imelenga Kuamsha ari na Muendelezo wa zao la mchikichi Kwa wakulima na wawekezaji wa zao hilo Mkoani Kigoma kwakuwa  mafuta yanachukua nafasi ya pili katika Kuingiza fedha za kigeni  na hivyo wakulima wakiongeza tija ya uzalishaji zao hilo litawainua.

"Waziri Mkuu  atawasili Mkoani Kwetu siku ya Jumamosi,na atatembelea Wilaya nne za Kigoma , Kasulu , Uvinza na Buhigwe katika ziara hiyo  itahusisha Kikao cha ndani na Viongozi wa Mkoa kufanya mkutano wa wadau wa zao la michikichi na  atatembelea wakulima wa Michikichi na kahawa ambapo atasikiliza kero za wakulima na kubadilishana nao mawazo", alisema Brigedia Jenerali Maganga .

Alieleza kuwa serikali imejipanga kuinua zao la mchikichi na kuwataka wamiliki wote wa mashamba ya michikichi ambayo hayatumiki  wayarudishe iliwaweze kupatiwa watu ambao wanaweza kuwekeza na kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Aidha Maganga aliwaomba Wananchi kujitokeza kwa Wingi katika mikutano  atakayo ifanya na kutoa kero zao kwa kufuata utaratibu na kuwasilisha mambo yote ambayo yameshindwa kutatuliwa na Viongozi wa  wilaya na Mkoa  waziwasilishe kwa Waziri Mkuu ziweze kutatuliwa kwa wakati.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: