Jeshi la Polisi mkoa wa Singida kwa kushirikiana na shirika la Sightsaver wameendesha zoezi la kuwapim a macho Madereva na kubaini kuwa kati ya madereva miamoja madereva kumi wanauoni hafifu ,jambo ambalo linaweza kuwa ni moja ya chanzo cha kusababisha ajali.
Hatua hiyo imefikiwa kwenye zoezi la siku kumi la mafunzo kazini kwa madereva na kuwapima macho na kubaini kati ya madereva elfumoja miatano na tatu walio kwishapimwa madereva miamoja na sitini na tano wamebainika wanauoni hafifu huku wakiendesha vyombo vya moto.
Awali kamanda wa Polisi mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba amesema baadhi ya ajali zimekuwa zikisababishwa na uoni hafifu kwa madereva, ndio maana jeshi la polisi likaamua kuwapima macho dereva wote wa mkoa wa Singida.
Kwaupande wake mratibu shirika lisilo la kiserikali la Sightsaver Bwana Edwin Maleko amesema toka waanze kutoa huduma za matibabu ya macho mwaka 2016,kwa zoezi la kupima madereva ni mara ya kwanza na wamekuta wagonjwa ni wengi,huku madereva waliopimwa wakipongeza zoezi hilo.
Post A Comment: