Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemhakikishia Rais John Magufuli kuwa atapambana na ajali za barabarani na kwamba zitapungua na kwisha kabisa ndani ya muda mfupi ujao.

Siku chache zilizopita wakati wa kuwaapisha mawaziri pamoja na viongozi mbalimbali aliowateua Magufuli alisema amechoka kutoa rambirambi kutokana na mfululizo wa ajali  za barabaran hususani Mkoa wa Mbeya.

Lugola amesema hayo  leo Julai 14 wakati Rais akimuapisha Kamishna Jenerali wa Jeshi la magereza Phaustine Kasike na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais na Muungano Joseph Sokoine viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.  

“Ulivyoniapisha yapo mambo ya msingi ambayo ulinielekeza niyafanyie kazi nataka nikuhakikishie mambo hayo nimeshaanza kuyafanyia kazi, pamoja na makatibu wangu,”amesema na kuongeza kuwa:

“Ili kuonyesha kwamba tumeyapa uzito na kuanza kuyatekeleza pasipo mzaha tayari kwenye upande wa ajali tumeshaanza kuchukua hatua na nataka nikuthibitishie kwamba utapata usingizi na hata salamu za pole zitapungua na zitakwenda kwisha kabisa ndani ya muda mfupi ujao.”

Kingine alizungumzia kuhusu  mikataba ya hovyo ya kifisadi na kulidhalilisha taifa.

“Hatuwezi kuwa na tuhuma za Watanzania zisizoisha na kuleta sintofahamu,  vitendo hivi lazima vifike mwisho, hivyo nakuahidi kwa kuwa umeniamini na mimi nitafanya kazi bila kujali nafasi ya mtu wala upendeleo,”amesema.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: