Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugolaamesema ifikapo saa 12 jioni leo atahitaji maelezo kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro kuhusu alipo mbwa maalumu wa polisi wa kikosi cha Bandari ambaye hajulikani alipo.

Lugola ametoa kauli hiyo leo, Alhamisi Julai 19, 2018 wakati alipofanya ziara Bandari ya Dar es Salaam, kwa ajili ya kuona utendaji kazi wa jeshi la polisi bandarini hapo.

Amesema kikosi kina jumla ya mbwa sita maalumu, wawili wapo mafunzoni na wanabaki wanne ambapo kati yao mmoja aitwaye Hobby hajulikani alipo.

Alisema ameulizia alipo mbwa huyo lakini haijulikani alipopelekwa wala alipolala tangu alivyoondolewa jana asubuhi.

Hivyo amesema akimaliza ziara yake leo, saa 12 jioni IGP Sirro yeye mwenyewe ampigie simu akiwa na huyo mbwa  pale polisi Bandari ili ajiridhishe  alikuwa wapi na alikwenda kufanya nini
Share To:

msumbanews

Post A Comment: