Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amewataka wakazi wa Arusha, kuonesha hasira zao za kuwa na maisha magumu kwa kuwachagua wagombea wa udiwani wa Chadema.

Akizungumza jana katika uzinduzi wa kampeni katika Kata ya Daraja Mbili, Lema alisema Chadema inaingia katika uchaguzi mdogo ili kuonyesha majaribu ambayo Taifa linapita kwa sasa licha ya hofu kutawala . 

"Katika uchaguzi huu, hatupambani na (Prosper) Msofe (mgombea wa udiwani wa CCM) ambaye alikuwa diwani wetu na tulipambana na damu kumwagika ili awe diwani lakini amejiuzulu na kujiunga na CCM, sisi tunapambana kwa ajili ya maisha ya Watanzania," alisema Lema

Alisema hivi sasa hali ya maisha ni ngumu, biashara nyingi zimefungwa, migodi imefungwa na maisha ni magumu na hakuna sehemu ya kuonyesha hasira hizo zaidi ya kutowapigia kura CCM.

"Hivi sasa akina dada warembo wanakunywa konyagi ukiwauliza vipi wanasema eti wanapunguza mafuta mwilini, lakini hapana, tatizo hali ni ngumu ya maisha," alisema

Hata hivyo, alisema tatizo kubwa la Watanzania ni woga, hawataki kusimama na kutetea ukweli jambo ambalo madhara yake yataendelea kuwa makubwa.

Aliwaomba wakazi wa Kata ya Daraja Mbili, kumpigia kura mgombea wa Chadema, Masudi Sungwa ili aendelee kuwasaidia kutatua kero zao.

Kwa upande wake,  Masudi Sungwa aliomba kura kwa wakazi wa kata hiyo na kueleza kero zao atazishughulikia vyema akishirikiana na baraza la madiwani wa Jiji la Arusha ambalo linaongozwa na Chadema.Mke u
Share To:

msumbanews

Post A Comment: