Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Hamisi Kigwangalla, amekiri kuwa usiku wa jana alipata tabu sana kwa wananchi wa Wilaya ya Tarime ambapo walimfanyia hujuma yakumuwekea misumari na kumpangia mawe barabarani akiwa na msafara wake ili wakawie kutoka ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Waziri Kigwangwalla alikutana na kadhia hiyo wakati akirudi kutoka kukagua mipaka katika eneo lenye mgogoro kati ya hifadhi na vijiji jirani ndani ya wilaya hiyo.

Waziri Kigwangalla amekiri hayo ikiwa leo ni siku yake ya tano katika ziara aliyoipa jina ya pori kwa pori ambapo kwa siku ya leo anaelekea kukagua mpaka wa Serengeti sambamba na kuangalia eneo walipouawa simba 9 kwa sumu.

Usiku wa kuamkia leo Waziri Kigwangalla akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Mara na viongozi wengine wa Serikali na kisiasa wilaya ya Tarime walilazimika kuteremka kwenye magari na kuanza kazi ya kuyaweka pembeni mawe hayo, ambapo pia walikusanya na misumari kazi iliyochukua zaidi ya saa 1.

"Hawa waliopanga mawe barabarani walitaka msafara wangu ulale porini, nimekuja kwa mapenzi mema kuona namna gani tutatatua mgogoro huu badala yake nazuiliwa kupita kwa kupangiwa mawe!,  Dk. Kigwangalla"

Tukio hilo la kupangiwa mawe kwa kiongozi huyo ni muendelezo wa matukio ya hatari anayokutana nayo ambapo mwanzo wa ziara yake akiwa katika  akiwa pori la msitu wa Patamela, Songwe wahalifu ambao walikuwa wakifanya ujangili katika machimbo ya madini walichoma moto msiu huo ili kumchelewesha Waziri huyo akawie kufika wnwo la tukio.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: