Kamishna  Jenerali wa Uhamiaji Tanzania, Dkt. Anna Makakala amewataka watanzania wote nchini kutoshiriki kuwahifadhi ama kuwasafirisha wahamiaji haramu kwa njia za panya katika maeneo yao.

Makakala ameyasema hayo leo mara baada ya kumaliza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Lindi, yenye lengo la kuzungumza na watumishi wa idara ya Uhamiaji juu ya maswala mbalimbali likiwemo la changamoto zinazowakabili.

Amesema Idara ya Uhamiaji iko makini kufuatilia kila kona ili kuwabaini wananchi wanaoshirikiana na wahamiaji na kwamba pindi watakapo wabaini sheria kali zitachukuliwa dhidi yao

“Sheria ya Uhamiaji kwa sasa imeongezewa makali, mtu atakayejihusisha na shughuli hiyo basi atatozwa faini isiyopungua shilingi milioni 20 au kifungo cha miaka 20 au vyote kwa pamoja, pia kutaifisha mali zote zitakazohusika kuwasafirisha wahamiaji hao”

Awali akisoma taarifa ya utendaji kazi ya Uhamiaji kwa Mkoa wa Lindi, Afisa Uhamiaji Mkoa, Abdallah Katimba amesema kutokana na doria zinazofanywa mara kwa mara katika nyumba za kulala wageni, vituo vya mabasi, barabara kuu ya Dar-es-salaam- Mtwara na njia za michepuko zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia na kupitia ndani ya Mkoa wa Lindi na kuelekea nchi za kusini mwa Afrika waliweza kukamata raia wawili wa Vietnam, watano wa Ethiopia na mmoja wa Malawi na kuwafikisha mahakamani kwa makosa mbalimbali ya kiuhamiaji.

Katimba aliongeza kuwa, kuwepo kwa Mkoa wa Lindi katika mwambao wa bahari ya Hindi pamoja na kuwa jirani mwa Nchi ya Msumbiji umesababisha raia wengi wa Msumbiji kuingia nchini Tanzania na kulowea kutokana na shughuli za kiuchumi, kijamii na kitamaduni.

“Kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika utowaji wa vitambulisho vya taifa , kwa lengo la kuwabaini wahamiaji wasio raia wa Tanzania ambalo linaendelea hadi sasa jumla ya watu 8,123 wasio raia wa tanzania wamefanikiwa kuwabaini katika ofisi ya uhamiaji mkoa na wilaya zake.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: