Mkurugenzi wa Kilimo na Mifugo katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Luteni Kanali Peter Lushika akitoa maelezo kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka, kuhusu Mabanda ya miifugo yaliyojengwa na jeshi hilo kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika Kitaifa, 2018 Uwanja wa Nyakabindi katika Halmashauri ya mji Bariadi .
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu kabla ya viongozi hao kutembelea eneo la jeshi hilo lililoandaliwa kwa ajili ya maonesho ya Nanenane lililopo katika Uwanja wa Nanenane uliopo Nyakabindi Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa na viongozi wa Mkoa huo kabla ya kutembelea eneo la jeshi hilo lililoandaliwa kwa ajili ya maonesho ya Nanenane lililopo katika Uwanja wa Nanenane uliopo Nyakabindi Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Kilimo na Mifugo katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Luteni Kanali Peter Lushika akitoa maelezo juu ya vipando vilivyoandaliwa na jeshi hilo kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka walipotembelea eneo hilo lililopo Uwanja wa Nyakabindi katika Halmashauri ya mji Bariadi.
Viongozi wa JKT na mkoa wa Simiyu wakiangalia moja ya mabwawa ya samaki yaliyoandaliwa na Jeshi la kujenga Taifa(JKT) kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Nanenane wa kanda ya ziwa mashariki, uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu akisaini vitabu vya wageni vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, kabla ya kuanza kutembelea eneo la jeshi hilo lililoandaliwa kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika kitaifa mkoani humo Agosti 2018, lililopo katika Uwanja wa Nanenane uliopo Nyakabindi Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akisisitiza jambo katika kikao kati ya viongozi wa Mkoa huo na viongozi wa JKT wakati wa ziara ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu katika eneo la jeshi hilo lililoandaliwa kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika kitaifa mkoani humo Agosti 2018, lililopo katika Uwanja wa Nanenane wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Kilimo na Mifugo katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Luteni Kanali Peter Lushika akizungumza na viongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa na viongozi wa Mkoa wa Simiyu kabla ya kutembelea eneo la jeshi hilo lililoandaliwa kwa ajili ya maonesho ya Nanenane lililopo katika Uwanja wa Nanenane uliopo Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.



Na Stella Kalinga, Simiyu

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu ameahidi kuwa Jeshi hilo litajenga Majengo ya kudumu katika Uwanja wa Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki wa Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu, ili kuendelea kutoa elimu ya teknolojia mbalimbali za kilimo na ufugaji kwa wakulima, wafugaji na wavuvi.

Meja Jenerali Busungu ameyasema hayo wakati alipotembelea eneo la JKT lililopo Uwanja wa Nanenane Nyakabindi kwa lengo la kujionea maandalizi hayo yanayofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa.Busungu amesema baada ya Nanenane wataanza ujenzi wa majengo ya kudumu ili wakulima, wafugaji na wavuvi wanufaike na teknolojia ya kilimo kwa muda wote.

“Mkuu wa mkoa ametupa mkakati wao kuwa kila baada ya miezi mitatu kutakuwa na maonesho katika uwanja huu, tunaahidi kujenga majengo ya kudumu hapa na maonesho yajayo miezi mitatu inayofuata wananchi watarajie kupata vitu vizuri kutoka JKT, maana JKT ni kisima cha kila kitu” alisema Meja Jenerali Busungu.

“ Katika maonesho haya watarajie kuona teknolojia mbalimbali za kilimo, ufugaji, uvuvi pia watarajie kuona bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na JKT zikiwemo bidhaa za kilimo, viwanda na kwa ndugu zangu Wanyantuzu wataona mbuzi na kondoo wa maziwa na wataona kuwa si ng’ombe tu wanaotoa maziwa” alisisitiza Meja Jenerali Busungu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru JKT kwa kazi kubwa ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane waliyoifanya, huku akibainisha kuwa uwepo wa JKT utasaidia kuwabaadilisha vijana wa Simiyu kwa kuwa watapata fursa ya kujifunza teknolojia mbalimbali.

“ Tunawashukuru sana JKT kwa kutuamini na tunajua kuwepo JKT kutasadia kuwabadilisha vijana wa hapa kwa kuwa kuna vijana wanamaliza darasa la saba au kidato cha nne hawana pa kushika na sisi tuna vikundi vingi vya vijana , tuko tayari kuleta vikundi vyetu vya vijana kuja kujifunza hapa” alisisitiza Mtaka.

Naye Mbunge wa Itilima amesema maonesho ya nanenane na uwepo wa JKT kutakuwa msaada kwa wananchi kwa kuwa watapata elimu itakayowawezesha kufanya uzalishaji wenye tija ikiwemo ufugaji wa kisasa na kilimo bora.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: