Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewapongeza viongozi wa wilaya ya Manyoni kwa kusimamia vyema fedha za serikali zilizowezesha kujenga vizuri sana kituo cha afya Kitinku.
Waziri Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayo tekelezwa chini ya ofisi ya Rais TAMISEMI.
Jafo ameridhishwa na ujenzi wa kituo cha afya Kitimku ambacho serikali ilipeleka shilingi milioni 500 ili kufanya uboreshaji na kujenga majengo mbalimbali ikiwemo jengo la huduma za upasuaji. Amesema kituo hicho kimekuwa mfano wa kuigwa.
Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amemshukuru Mbunge wa Jimbo hilo Mhe . Daniel Mtuka pamoja na Kaimu mkuu wa wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuiunganisha timu ya watendaji na wanajamii wa Manyoni.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akikagua jengo la upasuaji Kituo cha Afya Kintinku.
Baadhi ya majengo ya kituo cha Afya Kintinku.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akikagua chumba cha kuhifadhia maiti katika Kituo cha Afya Kintinku.
Post A Comment: