Ni ya kuchangia ujenzi wa madarasa iliyofanyika April, 2018. Yaanza kutumika ili kukamilisha madarasa 50 yaliyokusudiwa.
Kata 10 zilizokamilisha michango zakabidhiwa fedha za kukamilisha majengo. Uzinduzi wafanyika kata ya mabilioni, shule ya msingi Moipo.
Wadau wakumbushwa kukamilisha ahadi ili kazi hiyo ikamilike ifikapo Novemba, 2018.
Uzinduzi wa ujenzi wahudhuriwa na DC Same, Mwenyekiti Halmashauri, kaimu DED, Diwani, WEOs 10 na wataalamu.
" Ukamilishaji wa madarasa haya utawezesha watoto 2250 kupata madarasa ya uhakika ya kusomea" Alisema DC Same, alipokuwa akiwashukuru wote waliochangia.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri aliahidi kusimamia vizuri michango hiyo na kuwataka WEOs kutoa taarifa ya matumizi kwa wananchi.
Wananchi wahimizwa kuhakikisha watoto wanaenda shuleni ili kuunga mkono juhudi za Mh. Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli na serikali yake ya kutaka watoto wote wapate elimu bure, wale watoro wazazi wao kushughulikiwa.
" ELIMU BORA NI WAJIBU KILA MWANA JAMII"
Post A Comment: