Mshambuliaji mpya wa Simba, Adam Salamba amekutana na majanga baada ya gari lake kupata ajali na kuharibika vibaya.

Taarifa zinaeleza, gari hilo aina ya Toyota Crown lilikuwa njiani kutoka jijini Mwanza kwenda Dar es Salaam na likiwa katika foleni eneo la Mlandizi likagongwa na kuharibika vibaya.

Salamba amesema kwamba dereve alikuwa katika foleni na roli likafeli breki.

“Likaigonga gari nyuma, nayo ikaigonga gari nyingine. Kwa kweli limeharibika vibaya sana,” alisema Salamba akionyesha kuwa na masikitiko makubwa.

Salamba alipata gari hilo mara baada ya kutua Simba akitokea Lipuli ya Iringa.

Matarajio yalikuwa aanze kulitumia kuanzia juzi baada ya kutua Dar es Salaam.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: