Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mheshimiwa Idd Hassan Kimanta jana tarehe 11/07/2018 alizindua kiwanda kidogo cha kuchakata Ngozi na kutengeneza bidhaa za ngozi kiwanda hicho kipo katika kijiji cha Mswakini na kutoa vyeti kwa wanakikundi waliofuzu mafunzo.
kiwanda hicho ni matokeo ya kikundi cha akina mama 22 ambao mwezi Agosti 2017 walijiunga pamoja na kupata ufadhili kutoka shirikikala OIKOS kwa lengo kujijenga kiuchumi kupitia Ngozi na kuunga mkono Juhudi za Serikaliya kuelekea Tanzania ya Viwanda.
Katika halfa hiyo Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amewapongezakinamama hao kwa uamuzi wao huo na kuwahidi kuwa kupitia Halmashauri ya Wilaya Monduli atahakikisha wanapata Mkopo ili kuongeza mtaji.
Pia amelishukuru SHirika la Misaada la Marekani-USAID kwa kulipatia fedha shirika la OIKOS ambalo ndilo lililosimamia mchakato wote kupitia Mradi wa Ikolojia Hatarini Kaskazini mwa Tanzania.
Post A Comment: