Mkuu wa wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa Mh. Asia Abdallah Amekabidhi mifuko 20 ya cement kwa uongozi wa Kata ya Masisiwe kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya Msingi katika shule ya Idegenda Wilayani humo.

Dc Asia amekabidhi mifuko hiyo kwa Diwani wa kata hiyo Ndg. Vitalisi Kavela akiwa ameambatana na mwenyekiti wa kijiji sambamba na Mtendaji wa kijiji hicho ikiwa ni muendelezo wakuimarisha miundombinu ya shule kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ndani na nje ya Wilaya ya Kilolo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: