Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mh. Asia Abdallah amekanusha Taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna maporomoko ya mawe kwenye Mlima kitonga.

Akizungumza na Msumbanews Blog asubuhi ya leo ameeleza kuwa 

"Yawezekana yameporomoko ila siyo ndani ya Kilolo, Mipaka ya Kilolo na Milima Kitonga kwa kipindi cha hivi karibuni hakijapata hiyo ajali ya kuporomokewa na mawe, Jana, juzi vikosi vya usalama  na mwenyekiti wao wa Usalama vilikuwa na doria Mahenge- ILula Wilayani Kilolo na hapakuwa na hiyo ajali. Hata hivyo nawashauri watumiaji wa barabara hiyo kuendelea kuitumia kwa uangalifu kwa kuwa uwezekano wa mawe kudondoka upo kwani ni eneo Lenye Kona Kali na Milima yenye Mawe"
Share To:

msumbanews

Post A Comment: