Aliko Dangote
Dangote akihojiwa na gazeti la Financial Times (FT) amesema kwa sasa ana miaka 60 na yupo bize sana hawezi kutafuta mwanamke lakini akijitokeza wa kumuoa basi atafanya hivyo.
“Mimi sio kijana tena, miaka 60 sio masihala kwani siwezi kutembea mtaani kutafuta mwanamke nakosa muda kabisa lakini akitokea wa kuwa naye sawa,“amesema Dangote.
Tajiri huyo maarufu zaidi barani Afrika amesema kuwa kwa siku anapigiwa simu zaidi ya mara 100 huku akipokea maelfu ya barua pepe.
Dangote mpaka hivi sasa ameachwa na wanawake wawili na amefanikiwa kupata watoto watatu ingawaje vyombo vya habari nchini Nigeria vinaripoti kuwa Bilionea huyo ameshawahi kuishi na wanawake watatu baada ya kuachana na wanawake wake wa ndoa lakini hajafanikiwa kuzaa nao.
Chanzo: Financial Times (FT)
Post A Comment: