Msanii wa muziki wa hip hop, Chemical amewajia juu mashabiki ambao wanamkosoa namna anavyovaa nguo huku wengi wakidai anavaa sana nguo za kiume kuliko za kike.
Mrembo huyo ameonyesha kuchukizwa na kauli hizo hali ambayo imemfanya awatolee uvuvi wote ambao wamekuwa akimtupia maneno kuhusu munonekano wake wa mavazi.
“Kama kuna mwanaume anaweza kuvaa nguo zangu ajue kabisa sio mwanaume aliyekamili na atakua na matatizo,” aliandika rapa huyo kupitia instagram.
Aliongeza, “Na wewe ambaye kila ukikaa unajudge mavazi yangu na muonekano ujue unajipotezea muda navaa navyojisikia kuvaa na uwanamke wangu si wa mavazi..Upo nyonyo👌. Mwanaume kamili anajua mimi ni mwanamke. Kama huwezi kushabikia mziki wangu bila kuangalia mavazi hufai kua shabiki wangu pia..shenz type Mxiuuuw,”
Mwanadada huyo amekuwa aliandamwa sana mitandaoni kutoka na mavazi ambayo amekuwa aliyavaa.
Post A Comment: