Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinajipanga kuwasilisha malalamiko yake katika kamati ya Taifa ya maadili kutokana na kutoridhishwa na sababu za kuondolewa kwa baadhi ya wagombea wao.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumanne Julai 24, 2018 mkurugenzi wa uchaguzi wa Chadema, Reginald Munisi alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeshindwa kutoa sababu za kuondolewa kwa wagombea wa chama hicho katika kata tano za mjini Tunduma na kata ya Gangilonga manispaa ya Iringa.
“Tutapeleka malalamiko yetu katika chombo hicho na tusipopata msaada tutakwenda kamati ya maadili ya rufaa kabla ya kwenda mahakamani,” alisema
Post A Comment: