Diwani wa Kata ya Manuzi, Elias Shukia na dereva wa halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Haruna Ngata wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka koani Dodoma, kupasuka tairi na kupinduka mara tatu.

Taarifa za awali kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu zinaelea kuwa ajali hiyo imetokea  eneo la Mkiwa, Wilayani Singida.

 Mtaturu amesema mkuregenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Meatu,  Fabian Manuzi; mwenyekiti wa halmashauri hiyo,  Piuz Machungwa na watu wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali hiyo.

Amesema majeruhi wanne wamelazwa katika hospitali ya St Gasper iliyopo Itigi na wawili wamelazwa hospitali ya Puma iliyopo wilayani Ikungi.

“Chanzo tulichokiona kwenye eneo la tukio ni kupasuka kwa tairi la mbele kushoto, hata hivyo tuwasubiri polisi wafanye uchunguzi zaidi watatuambia chanzo cha ajali yenyewe,”amesema.



Share To:

msumbanews

Post A Comment: