Mbunge wa Singida magharibi Mh: Elibariki Kingu Akimpokea Katibu kata wa chadema Ndg. Daudi Juma  baada ya kujiunga na Ccm.

Zaidi ya wanachama 70 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wengi wao wakiwa viongozi wa matawi mbali mbali  wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM katika Jimbo la Singida Magharibi mkoani Singida.

Maamuzi ya wanachama hao yametokana na maendeleo yanayoletwa  katika Jimbo hilo ambayo yanafanywa na Mbunge wa Jimbo hilo Mh: Elibariki Kingu.

Katibu kata wa Chadme ambaye ndio kiongozi wa Wanachama hao  ambao wamekihama Chama cha CHADEMA na kujiunga na CCM, akielezea  sababu za kukihama chama hicho katika mkutano wa Hadhara wa Mbunge Kingu   ambao umefanyika katika viwanja vya kata ya Iseke katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida ameeleza kuwa  
"mabadiliko yaliyoletwa ndani ya Jimbo hilo kwa ndani ya miaka miwili ni mengi sana hivyo hana budi kuendelea kumpinga mbunge kwa kuwa amewaletea umeme kwa kila kijiji na maji kwa kipindi kifupi hivyo hawezi kubaki tena upinzani kwa mambo aliyokuwa anapigania yafanywe na Chadema sasa yanafanywa kwa ka."


Wakizungumza katika mkutano huo huku wakirudisha kadi za CHADEMA, wanachama hao wame

Wanachama wa Chadema wakila kiapo cha kujiunga chama cha Mapinduzi  mbele ya Mbunge wa Singida Magharibi Mh: Elibariki Kingu katika Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Ikungi akiwa ameshikilia  baadhi ya kadi za wanachama.
Katibu kata wa chadema Ndg. Daudi Juma akikabidhi kadi kwa Mwenyekiti wa Ccm Wilaya.
Mwenyekiti wa Ccm Kata ya Iseke akimpokea mmoja wa wanachama wapya waliojiunga na Ccm.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: