Wakati Yanga wakihaha kum­bakisha beki mkongwe wa kati, Kelvin Yondani watani wao wa jadi Simba nao wame­ingia rada za kuhakikisha wanainasa saini ya nyota huyo.

Beki huyo, hivi sasa ni mchezaji huru anayeruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu yoyote itakayomhitaji kwa ajili ya kuichezea katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara baada ya mkataba wake ku­malizika mwezi huu Mei.

Yondani ni kati ya mabeki bora katika msimu huu wa ligi kutokana na kucheza vema katika nafasi hiyo ya kati am­bapo hivi sasa anawindwa na timu kadhaa ikiwemo Azam FC.

Kwa mujibu wa taarifa am­bazo imezipata uon­gozi wa Yanga, wana taarifa za beki huyo kuwindwa na Simba kwa ajili ya kumsajili na kinachowachanganya zaidi ni kutokuwepo kambini pamoja na wenzake.

Mtoa taarifa huyo alisema, beki huyo tayari amewaam­bia viongozi wa timu juu ya kuwindwa na Simba baada ya kupokea simu nyingi kutoka kwa mabosi wa Msimbazi kuonyesha nia ya kumsajili.

“Sisi wenyewe Yanga ndiyo tunamuwekea mazingira ya kuondoka Yondani kwenda Simba, kwani tayari ameutaar­ifu uongozi juu ya usumbufu anaoupata kutoka Simba, la­kini wenyewe wanakaa kimya.

“Kama kusaini mkataba Simba angekuwa ameshaini mkataba muda mrefu, lakini mwenyewe ameonekana ku­totaka kuondoka kwa kuhofia kujirudia kile kilichompata akiwa anaichezea Simba kabla ya kuja Yanga.

“Yondani hakujiunga na msafara wa timu ya Yanga uliokwenda Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika na sababu ikiwa ni nyepesi kuwa alipata majeraha mechi na Simba kitu ambacho siyo kweli, hivyo viongozi wa Yanga waangalie asije akaondoka,” alisema mtoa taarifa.

Alipotafutwa Yondani hakupatikana, lakini beki huyo hivi karibuni aliwahi kuzungumzia hatma yake: “Mimi mkataba wangu un­amalizika mwezi Mei, hivyo baada ya hapo nitakuwa huru kusaini timu yoyote.”

Alipotafutwa baba yake, Yondani, mzee Patrick Yonda­ni kuhusu mwanaye alisema: “Mimi ninachojua aliniambia anaumwa, aliumia katika mechi ya Simba, kuhusu yeye kutopatikana sijawasiliana naye baada ya kunipa taarifa hizo na sijui kama ni kweli amewagomea kusafiri.”

Hadi muda wa jioni kikosi cha Yanga kilipokuwa kikion­doka Dar, uongozi wa timu hiyo haukujua alipo mchezaji huyo kwa kuwa hata simu yake haikuwa ikipatikana hewani.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: