Uongozi wa Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga umeeleza sababu zilizopelekea jezi zao kutokuwa na nembo ya wadhamini ambayo ni kampuni ya kubashiri matokeo ya SportPesa wakati wa mchezo wao wa hapo jana dhidi ya USM Alger ya nchini Algeria michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF. 
Taari yao kwa vyombo vya habari hii leo Yanga imesema kuwa walizuiwa kutumia jezi hizo zenye nembo ya SportPesa kwasababu ni kukosekana kwa maelekezo ya matumizi ya wadhamini hapo awali na hivyo kulazimika kuzibwa kwa sehemu hiyo.
Yanga akiwa ugenini nchini Algeria ilikubali kipigo cha mabao 4 – 0 kutoka kwa wenyeji wao timu ya USM Alger mabao yakifungwa na Darfalou dakika ya nne, Chafai akifunga dakika ya 32, Meziane akitupia dakika ya 54 na lamwisho likiwekwa kimyani na Zemmamouche dakika ya 93.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: