Klabu ya Yanga imefanya mkutano wake wa mwisho na waandishi wa habari jana nchini Algeria kabla ya kushuka dimbani hapo leo hii kuivaa USM Alger mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Yanga itashuka dimbani kuwakabili USM Alger mchezo wa kwanza wa kundi D utakao pigwa majira ya saa 4: 00 usiku majira ya Afrika Mashariki.
Kikosi cha mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga kimesafiri juzi kuelekea nchini Algeria kwaajili ya mchezo wa kwanza wa makundi dhidi ya USM Alger utakao pigwa hapo kesho siku ya Jumapili huku wachezaji wake nyota, Ibrahim Ajib, Obrey Chirwa, Papy Kabamba Tshimbi na Kelvin Yondani wakikosekana kwenye kikosi hiko kwa sababu mbalimbali.
Post A Comment: