Winga wa kimataifa wa Tanzania anaecheza soka la kulipwa nchini Morocco kwenye klabu ya Difaa El Jadidi, Simon Msuva ametembelea kambi ya timu yake ya zamani ya Yanga kwaajili ya kuwapa wachezaji wenzake moyo kuelekea mchezo wao wa hapo kesho dhidi ya USM Alger ya Algeria kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Msuva yupo nchini Algeria kwaajili ya mchezo wao wa klabu bingwa Afrika dhidi ya MC Alger uliyopigwa hapo jana siku ya Ijuma na kumalizika kwa sare ya bao 1 – 1.
Baadhi ya picha zikimuonyesha Msuva akisalimiana na wachezaji wengine wa Yanga pamoja na baadhi ya viongozi.
Post A Comment: