Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kuelezea mipango yake  aliyonayo kuhusu  kipindi chake  kinachotarajiwa kurushiana ndani ya Wasafi Tv.

Kama utakumbuka siku za nyuma kidogo Wema aliweka wazi kuwa hana Mahusiano ya kimapenzi na Diamond bali atakuwa na uhusiano wa kikazi naye kwani atakuwa bosi wake.

Wema alitangaza kuwa atakuwa na kipindi ndani ya Wasafi Tv ambayo imeanza kurusha matangazo yake wiki chache zilizopita.

Wema amefunguka hayo kwenye press conference aliyofanya kuweka wazi kitakuwa ni kipindi cha kawaida na sio reality show kama ilivyokuwa mwanzoni kwenye EATV.

"Kitakuwa ni kipindi cha tofauti tutakuwa wanadada watatu. Sitapenda kuweka wazi zaidi lakini haitakuwa reality show, kama itakuwa ni reality show nitaweka kwenye App yangu.

"Bado hatujaanza ku-shoot kwa sababu sasa hivi bado wanafanya majaribio, kwa hiyo ile process nzima ya vipindi bado haijanza, so content zipo pale pale na tutaanza ku-shoot hivi karibuni”.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: