WAZIRI wa Mambo ya Nje kutoka nchini Ujerumani Heiko Maas (Pichani), jioni ya leo Mei 3,2018 anatarajiwa kuwasili nchini kwa ajili ya kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili, ambapo anatarajiwa kulakiwa na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Agostino Maige na kufanya mzungumzo baina ya ushirikiano wa nchi hizo mbili.
Awali, akizungumza jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika Jestas Nyamanga alibainisha kuwa Waziri huyo katika ujio wake nchini ataambatana na ujumbe wa watu 50, ambapo lengo la ziara hiyo ni kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Ujerumani.
Waziri Maas amesema atakapowasili atapokelewa na kufanya mazungumzo akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga.
“Hii itakuwa ni ziara yake ya kwanza kuja hapa nchini na bara la Afrika tangu alipoteuliwa katika wadhfa huo, Machi 14, mwaka huu ambapo awali alikuwa Waziri wa Sheria nchini Ujerumani.
Mbali na Tanzania Waziri huyo awali alianza ziara yake nchi ya Ethiopia ambayo ni Makao Makuu ya Umoja wa nchi huru za Afrika (AU), hali hii inaonesha kuzidi kuimarika dhamira ya ushirikiano wa Mataifa haya mawili.
Kaimu Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa katika ziara hiyo Mei 4, Waziri Maas anatarajia kuweka shada la maua kwenye mnara wa askari uliopo katikati ya jiji kisha atatembelea Shule ya Sekondari ya Majaribio iliyopo Chang’ombe Manispaa ya Temeke ambapo atazungumza na baadhi ya wanafunzi wanaofundishwa lugha ya Kijerumani.
Nyamanga amesema siku hiyo Maas atasafiri hadi Mkoani Arusha ambapo atafanikiwa kukutana na viongozi mbalimbali wa mahakama ya kesi, Masalia ya mauaji ya Kimbari (MICT), na Mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu na watu.
Ametaja maeneo mengine Waziri huyo atakayotembelea kabla ya kuondoka nchini ni pamoja na Ofisi za Makao Makuu ya Jumuia ya Nchi za Afrika Mashariki (EAC), pamoja na maeneo mbalimbali yenye vivutio.
Hata hivyo amesema kuwa tangu ushirikiano wa Mataifa haya mawili ulipoanza miaka mingi iliyopita, nchi yetu imekuwa ikinufaika katika sekta tofauti tofauti zikiwemo Afya, elimu, Miundombinu, nishati mbadala pamoja na mapambano dhidi ya vitendo vya ujangili na uwindaji haramu.
Post A Comment: