Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas ametembelea Ofisi za Umoja wa Mataifa ya kushughulikia Masuala yaliyoachwa na Mahakama za jinai za umoja wa mataifa pamoja na kujionea makavati yaliyowekwa kumbukumbu za upelelezi,mashtaka na mwenendo wa kesi.

Waziri huyo aliambatana na  balozi za Ujerumani nchini Tanzania alipokuwa katika ziara yake ya siku moja ambapo alipata kujulishwa juu ya shughuli za za taasisi hiyo ambayo imejikita katika kuwasaka watuhumiwa ambao bado hawajakamatwa ,kuwalinda waathirika na mashahidi wa mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda.

Ziara ya waziri huyo ni ziara ya kwanza barani Afrika  tangu ateuliwe kuwa waziri march 2018 ,ziara hiyo ni muendelezo wa Nchi ya Ujerumani ambapo amesema kuwa wanafurahi  katoa mchango kwa taasisi hiyo ya kimataifa pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya  Ujerumani na bara la Afrika.

Afisa Mkuu wa Mambo ya nje katika taasisi hiyo  Ousman Njikam amemkaribisha Waziri huyo katika jengo la mahakama ambapo shughuli za kimahakama zinaendeshwa ,mahakama hiyo inaendelea na kazi yake ili kutoa haki kwa walalamikaji na walalamikiwa .

Msimamizi Mkuu wa Msajili wa Mahakama Sera Attika amesema kuwa mahakama hiyo ina sehemu maalumu za maabusu,na maktaba yenye makavati yaliyobeba historia ya Mauaji ya Rwanda ambayo hutumika kwa utafiti .



Waziri huyo ametembelea taasisi za kimaitaifa ikiwemo Mahakama ya Haki za binadamu ya Afrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: