Prof. Joyce Ndalichako ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwasaka watu wanaosambaza kitabu mitandaoni  chenye picha ya mwili wa binadamu huku kikiwa kimekosewa  na kuongeza kwamba watu hao wana nia ya kuichafua serikali.

Uamuzi huo umetolewa katika mkutano wa kumi na moja wa Bunge la Jamhuri ya muungano unaoendelea jijini Dodoma unaojadili mapendekezo ya bajeti ya mapato na matumizi ya wizara mbalimbali kwa mwaka 2018/19.

Prof. Ndalichako amesema kuwa kitabu cha kiingereza cha darasa la tatu kinachosambaa mtandaoni kilikuwa na makosa na kilisharekebishwa huku wahusika wakichukuliwa hatua lakini kitabu kinachoonyesha picha sehemu za mwili wa mwanadamu ni kitabu ambacho hakitambuliki na serikali hivyo wanaokisambaza watafutwe na wachukuliwe.

Hata hivyo Waziri Ndalichako ametoa hatua hiyo ikiwa ni baada ya Mbunge wa viti maalum, Martha Mlata, kuomba serikali itoe ufafanuzi kuhusu tukio hilo.

Aidha Katika majadiliano ya bajeti ya wizara ya elimu baadhi ya wabunge wameishauri serikali kufanya maboresho ya mitaala ya kufundishia.

Mbali na hayo serikali imeahidi  kulipa deni la shilingi trilioni 1.2 linalodaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii baada ya mpango wa serikali wa kuunganisha mifuko ya jamii utakapokamilika
Share To:

msumbanews

Post A Comment: