Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako Leo ametembelea na kukagua hatua za mwisho za usimikaji wa vifaa mbalimbali ndani ya maabara ya kisasa ya Kuhakiki vifaa vinavyopima mionzi katika Tume ya nguvu za Atomiki- TAEC iliyopo mkoani Arusha.
==>> Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>
Akizungumza mara baada ya kutembelea maabara hiyo Waziri Ndalichako amesema serikali imejenga maabara hiyo ya kisasa ili kudhibiti masuala ya mionzi kwa nchi za Afrika.
Alisema maabara hiyo ambayo sasa ipo katika hatua za kufungwa vifaa mbalimbali vya kisasa itawezesha nchi mbalimbali kuja kujifunza namna ya kupima masuala mbalimbali ya mionzi .
Waziri Ndalichako amesema kuwa hadi sasa serikali imeshatoa kiasi cha sh. bilioni 2.38 huku Umoja wa Ulaya (EU) ikitoa vifaa vyenye thamani ya sh. bilioni 11.
Imetolewa na;
kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
9/05/2018
Post A Comment: