Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema maamuzi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji ni sahihi na ameyafanya kwa wakati muafaka.
Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Bibi Felista Bura (Viti Maalumu) aliyetaka kupata kauli ya Serikali juu ya baadhi ya watu wanaobeza maamuzi ya Rais Magufuli ya kuupandisha hadhi mji huo.
“Pia Dodoma inajitosheleza kwa mahitaji mengi ikiwemo uwepo wa taasisi mbalimbali muhimu kama Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, vyuo vikuu zaidi ya vitano, Ofisi ya UN, hivyo nampongeza Mheshimiwa Rais Dkt Magufuli kwa uamuzi wake kwani unaleta tija kwa wananchi. Nashauri jambo hili lipongezwe badala ya kubezwa,” alisema Waziri Mkuu.
Aprili 26, 2018 Rais Magufuli aliupandisha hadhi mji wa Dodoma kutoka Halmashauri ya Manispaa na kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma pamoja na kumteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Bw. Godwin Kunambi kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: