Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewapiga marufuku wafanyabiashara wote nchini kupandisha bei ya sukari pamoja na bidhaa nyingine katika kipindi ambacho waumini wa kiislamu wanakuwa katika ibada ya kufunga mwezi wa Ramadhani unaotarajiwa kuanza siku si nyingi kutoka sasa ndani ya mwezi huu Mei.

Waziri Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Mei 03, 2018 Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 21 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la nyongeza la Mbunge Abdallah Bulembo aliyetaka kusikia tamko la serikali juu ya tatizo la sukari kuelekea mwezi wa ramadhani

"Suala la sukari tumelitafutia ufumbuzi tukiwa tunalenga kwanza upatikanaji wa bidhaa yenyewe iwe ya kutosha na kila mwenye mahitaji ya matumizi ili aweze kuipata sukari kwa urahisi ikiwemo na waislamu wanaoanza kufunga mwezi wa Ramadhani siku chache zijazo. Tunajua kila mwaka huwa tuna upungufu wa sukari lakini utaratibu tunaotumia ni kutoa vibali vya kuingiza sukari nchini ili kuweza kufanya soko la sukari kuendelea kuwepo na kufanya hivyo inasaidia hata bei za ndani kupungua"

Waziri Mkuu ameendelea kusema

"Kwa hiyo nataka niwaondolee mashaka watanzania na hasa waislamu kama ambavyo Mhe. Bulembo amesema kwamba sukari itapatikana kipindi chote cha ramadhani na maeneo yote ambayo yanahitaji sukari, pia tutaendelea kufuatilia muenendo wa bei ili watu wasiweze kupandisha bei ya sukari kwa makusudi tu kwa sababu watu wanajua mahitaji ya sukari yatakuwa makubwa kwa kufunga ramadhani".

Pamoja na hayo, Waziri Mkuu ameendelea kwa kusema "hili nalo tutalifanyia ufatiliaji kwenye maduka kwa sababu tumeweka utaratibu kusiwe na mtu yeyote anayeweza kupandisha bidhaa ya aina yeyote ile wakati wa ramadhani kwasababu kwa kufanya hivyo atakuwa anawaadhibu waislamu ambao wanaofunga ramadhani kwa sababu tu mahitaji yanakuwa makubwa".

Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema wameilekeza TRA vizuri kuwa wasitumie nguvu wala lugha chafu katika kukasanya kodi kwa wafanyabiashara nchini na kuwataka wafanyabiashara wote wawe na amani katika kufanyakazi zao pamoja na wawekazaji
Share To:

msumbanews

Post A Comment: