Waziri Mkuu,Kasimu Majaliwa, Mei 24 mwaka huu anatarajiwa kufungua vituo vitatu vikubwa vya Polisi katika maeneo ya Mburahati, Kiluvya na Mbweni jijini Dar Es Salaam.
Akizungumzia uzinduzi huo,Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro alisema kuwa vituo hivyo ni mafanikio ya ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi na wananchi katika mapambano dhidi ya uhalifu.
Aidha, amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ambao utaanzia katika kituo cha Polisi Mburahati na kufuatiwa na kituo cha Kiluvya na mwisho kituo cha Polisi Bweni.
Post A Comment: