Kampuni ya mtandao wa Twitter imewaonya watumiaji wake wapatao milioni 340 duniani kote kuwa wabadilishe nywira (password) zao kwa kile walichoeleza kuwa kwenye mfumo wao wa uendeshaji kumeingiliwa na kirusi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Twitter zimeeleza kuwa kuingiliwa huko kumesababisha password za watumiaji kuonekana kwa maandishi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Twitter, Jack Dorsey ameomba radhi kwa watumiaji wote kwa usumbufu huo wa kiufundi uliojitokeza.
Post A Comment: