Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule amethibitisha kufariki kwa wagonjwa saba wa kipindupindu katika Wilaya ya Sumbawanga huku wagonjwa wengine 44 wakibaki wodini kuendelea kupatiwa matibabu na wagonjwa 115 wakiruhusiwa kurudi nyumbani.

Akizingumzia tukio hilo Dkt. Haule amesema kuwa ugonjwa huo umelipuka Mei 6, 2018 katika Kijiji cha Mayenje, kata ya Milepa katika bonde la Ziwa Rukwa na kusambaa katika maeneo mengine ya Wilaya na hatimaye kupatikana kwa wagonjwa wawili katika hospitali ya rufaa ya mkoa.

"Sasa hivi katika bonde la ziwa Rukwa kuna shughuli za uvunaji wa mpunga na hivyo watu wengi hutokea huku juu kwenda bondeni kutafuta vibarua vya kuvuna mpunga kwenye maeneo hayo yaliyoathirika na kipindupindu, maji yanayotumika huko ni machafu kutoka katika madimbwi na mito. Nawaomba viongozi wa dini watoe tahadhari kwa waumini hasa katika maeneo yale yalioathirika zaidi", amesema Dkt. Haule.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: