Kwa mujibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, idadi ya watalii walioingia Tanzania imeongezeka kutoka Milioni 1.2 kwa mwaka 2016/17 hadi kufikia watalii milioni 1.3, huku watalii kutoka nchini Marekani wakiwa vinara.
Mapato yaliyopatikana kutokana na watalii hao yameongezeka kutoka wastani wa Dola za Kimarekani Milioni 2.1 hadi kufikia Dola Milioni 2.2.
Mapato yaliyopatikana kutokana na watalii hao yameongezeka kutoka wastani wa Dola za Kimarekani Milioni 2.1 hadi kufikia Dola Milioni 2.2.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudance Milanzi ambapo ameeleza Tanzania inazidi kufanya vizuri katika sekta ya utalii, huku idadi kubwa ya watalii wanatoka Marekani, Uingereza, India, Uholanzi na Uswiswi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza wakati wa uzinduzi wa taarifa hiyo. Kulia ni Kamishina wa Idara ya Uhamiaji, Hannelore Manyanga na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Takwimu ya Taifa (NBS) Dkt. Albina Chuwa.
Ripoti hiyo ya pamoja imeandaliwa kwa ushirikiano wa Benki Kuu Tanzania(BOT), Tume ya Taifa ya Takwimu (NBS), Idara ya Uhamiaji Zanzibar.
Kwa mujibu wa Milanzi, ripoti hiyo ilikusanywa kupitia viwanja vya ndege vya Julius Nyerere International Airport (JNIA), Kilimanjaro International Airport (KIA) na Abeid Amani Karume International Airport. Pia katika mipaka ya Namanga, Tunduma, Mtukula na kwingineko.
Post A Comment: