Zaidi ya wananchi wa elfu moja katika vijiji vinne vilivyopakana na hifadhi ya wanyamapori ya serengeti katika wilaya Tarime wamemuomba Rais Dkt John Pombe kuingilia kati mgogoro wa mpaka baina yao na Hifadhi ya Taifa TANAPA uliodumu zaidi ya miaka Hamsini kufuatia kuwepo upimaji holela wa mpaka huo bila kuwashirikisha wananchi .

Wananchi hao wamejitokeza kupinga uamuzi uliotolewa na  mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima wa kuwataka wananchi hao kupisha eneo la hifadhi ndani ya siku sitini huku wakiwa hawana mahali pa kwenda ,ambapo wametupia lawama serikali ya wilaya na mkoa kuchukua maamuzi hayo

Warioba mwita pamoja na Samweli Sauli ni ni moja ya wananchi wakieleza katika mkutano wa hadhara uliyofanyika katika kijiji cha kegonga wilayani Tarime mkoani Mara wakati walipomzuia mwenyekiti wa CCM Wilaya kupita na kumuomba asikilize kero zao wakati akielekea katika eneo la hifadhi ili kushuhudia malalamiko ambayo yametolewa na wanachi waishio katika eneo hilo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: