Mei 03 kila mwaka wanahabari na wadau wa habari huungana pamoja kuadhimisha “Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani” ambayo iliasisiwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1993.
Pamoja na mambo mengine, maadhimisho haya hulenga kutambua mchango wa vyombo vya habari pamoja na kuwakumbuka wanahabari waliopata madhara kutokana na kazi zao.
Jijini Mwanza, baadhi ya wanahabari wamekuwa na maoni tofauti kuhusiana na maadhimisho haya ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma yakiambatana na kaulimbiu isemayo “Wajibu wa Uongozi, Vyombo vya Habari, Haki na Utawala wa Sheria”.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: