Jumla ya wanafunzi 1,225 wa kidato cha sita, wanaanza mitihani yao taifa leo katika shule kumi za sekondari, halmashauri ya Arusha.
Afisa Elimu Sekondari halmashauri ya Arusha, mwalimu Sophia Msofe amethibitisha kuwa jumla ya wanafunzi 1,225 wanaanza mitihani hiyo, na kufafanua kuwa kati ya hao, wanafunzi 947 ni wa shule (School Candidates) na wanafuzi 278 ni wa kujitegemea (Private Candidates).
Ameongeza kuwa wanafunzi wa shule watafanya mitihani kwenye shule sita na wanafunzi wa kujitegemea watafanya mitihani kwenye vituo vinne vilivyo kwenye shule za sekondari Ilboru, Winning spirit, Enaboishu na Bishop.
Aidha Afisa Elimu Msofe amethibitisha kwa, maandalizi yote yamekamilika na mitihani itafanyika kulingana na ratiba ya mitihani iliyotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).
Hata hivyo Afisa Elimu huyo, ameongeza kuwa kati ya shule mbili kati ya shule kumi, zinazofanya mtihani leo, shule hizo zinafanya mtihani huo kwa mara ya kwanza.
Amezitaja shule hizo ni Mlangarini sekondari na Mwandeti sekondari, ambazo zilianza kupokea wanfunzi wa kidato cha tano kwa mara ya kwanza mwaka 2016.
Uongozi wa Halmashauri ya Arusha unawatakia kila la kheri wanafunzi wote wa kidato cha sita wanaoNza mtihani yao leo, waweze kufanya vizuri na kupata matokeo mazuri kwenye ufaulu.
Post A Comment: