Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kusema kuwa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanatamani sana yeye aonekane anaiunga mkono serikali ya awamu ya tano na kusema kuwa watasubiri sana kwa jambo hilo.
Msigwa amesema hayo leo Mei 3, 2018 baada ya moja ya video yake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuoonyesha akimsifia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa katika kipindi chake amekuwa hajali vyama kwani hata wao watu wa CHADEMA wamekuwa wakipokea fedha ambazo zimewawezeshja kujenga barabara kutoka Mlandege mpaka kwa Mkuu wa wilaya ambayo imegharimu zaidi ya bilioni tatu, wana stendi ya Ipogolo ambayo nayo imegharimu zaidi ya bilioni tatu na kudai kuwa Rais hapendelei.
Baada ya video hiyo kusambazwa sana Mchungaji Msigwa amesema kuwa "Vijana wa CCM wanatamani sana nionyeshe naiunga mkono serikali ya awamu ya tano! (Dying for my endorsement ) Mtasubiri sana"
Post A Comment: