Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amesema tangu rafiki yake Agnes Gerald ‘Masogange’ atangulie mbele ya haki amekuwa akihofia kutokewa na mzuka wake.
Uwoya ambaye alikuwa na ukaribu mkubwa na rafiki yake marehemu Msasogange amekiri kuwa tangu msiba huo amekuwa na hofu hata ya kukaa mwenyewe.
Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni na Global Publishers , Uwoya alisema, kwa jinsi walivyokuwa karibu na Masogange, amekuwa akiwaza mengi na ndiyo maana ameshindwa kabisa kuishi katika nyumba ile waliyokuwa wanaishi jirani na mrembo huyo, maeneo ya Makongo Juu jijini Dar.
"Nahofia kweli jamani kutokewa na Masogange. Kwa sasa imenibidi niwe mtu wa kujichanganya sana ili nisiwe namkumbuka Masogange”.
Masogange aliaga dunia wiki chache zilizopita baada ya Kuugua na kulazwa katika hospitali ya Mama Ngoma na kisha baadae kuzikwa kijijini kwao Mbeya.
Post A Comment: