Mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea leo Bungeni mjini Dodoma, likiwa limeongozwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai. Tazama picha za Wabunge mbalimbali wakiwa katika kipindi cha maswali na majibu.
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri mkuu Bungeni leo Jijini Dodoma
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza kikao cha ishirini na sita cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akimsikiliza Mbunge wa Songea Mjini Mhe Dkt Damas Ndumbaro wakati wa kikao cha ishirini na sita cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu akitolea ufafanuzi masuala mbalimbali ya Nishati wakati wa kikao cha ishirini na sita cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dk.Harrison Mwakyembe akimskiliza Mbunge wa Sumve Mhe.Richard Ndassa Bungeni leo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage akionyesha kitabu chenye idadi ya Viwanda vyote nchini wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2018/2019.Kitabu hicho kina kurasa mia tisa
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dk.Harrison Mwakyembe na Mbunge wa Sumve Mhe.Richard Ndassa wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya maudhui ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA) walipomtembelea leo Bungeni
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dk.Harrison Mwakyembe akimskiliza Mbunge wa Sumve Mhe.Richard Ndassa Bungeni leo Jijini Dar es Salaam
Post A Comment: