Mbunge wa Mfenesini, (Kanali mstaafu) Masoud Khamis amesema kuwa tatizo lililopo Tanzania kuanzia viongozi wote mpaka wananchi wa kawaidi ni kila mtu kujifanya ni polisi na anaijua kazi hiyo.
Mbunge Masoud ameyasema hayo leo Bungeni wakati akichangia katika sekta ya Wizara ya Mambo ya Ndani ambapo amesema kuwa kazi ya Polisi ni kazi ya Kitaalam ni kazi inayotaka mtu ajifunze na afanye vile inavyotakiwa
“Muheshimiwa Mwenyekiti tatizo tulilonalo Tanzania kuanzia sisi viongozi hata Wananchi wa kawaida kila mtu anajifanya yeye Polisi kila mtu anaijua kazi ya Polisi nataka niwaambie kazi ya Polisi ni kazi ya Kitaalam kazi inataka mtu ujifunze, ajue jukumu lake na afanye vile inavyotakiwa, utamkosoa polisi wewe kazi huijui, huwezi kufanya kazi ya Polisi kama wewe hujafunzwa ni kazi inayohitaji ujuzi na utaalam wa hali ya Juu sana na upelelezi ni kazi kubwa ambavyo hatuwezi kuvijua katika Bunge hili,” amesema Masoud.
“Polisi mi naomba hasa IGP mi naomba ufanye kazi yako kulingana na Katiba na sheria wala usiogope kitu wewe nakuona ni dereva mzuri, dereva mzuri aliebeba abiria ni yule ambae akisimama mahali ambapo hapa stahiki akipigiwa debe na kondakta hasimami mahali pasipo stahiki hasimami, dereva mnbaya ni yule ambaye anasimama mahali ambapo apa stahiki akasimama akasababisha ajali na vifo na mambo kadhaa, Kamanda Sirro endelea na kazi yako usibabaishwe na wapiga debe ambao hawafahamu nini wanachokifanya.
Post A Comment: