Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeibuka na kukanusha vikali kuwa kitabu kinachosambazwa katika mitandao ya kijamii kinachoelezea viungo vya mwanadamu sio chapisho la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na wala sio miongoni mwa vitabu ambavyo vimesambazwa shuleni.
Hayo yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kupitia Wizara ya Elimu Mwasu Sware hii leo Mei 04, 2018 baada ya kusambazwa picha hiyo katika mitandao ya kijamii na kupelekea kuzua mjadala mzito kwa wazazi pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu nchini jambo ambalo wamedai ndiyo sababu pekee ya elimu ya Tanzani kudidimia.
"Kitabu hicho hakina uhusiano wowote wala hakifanani na vitabu ambavyo vimechapishwa hivi karibuni na TET. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawasihi watanzania kupuuza taarifa hizo ambazo siyo za kweli na zina nia ya kupotosha na kuleta usumbufu kwa jamii", amesema Sware.
Soma hapa chini habari kamili kuhusiana na taarifa ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Post A Comment: