Kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam na mikoa ya Pwani kuanzia jana wamepata neema ya mvua ambazo zinaendelea kunyesha mpaka hivi sasa kitu ambacho kimepelekea baadhi ya maeneo ya jiji kukubwa na mafuriko, Sasa habari kubwa ni kwamba neema hiyo ya mvua itaendelea kumiminika tena kwa siku ya kesho Jumamosi Mei 05, 2018 hii ni kwa mujibu wa TMA.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 04, 2018 na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kesho Mei 5, 2018 mvua hizo zitaendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es salaam na mikoa ya Pwani, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba na kuambatana na upepo mkali.
TMA imetoa tahadhari ya mafuriko kutokea katika maeneo ya mabondeni, kuvurugika kwa usafiri na barabara kubwa kuharibiwa na mvua hiyo.
Hata hivyo, mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam tayari zimeanza kuleta madhara makubwa ikiwemo kuharibu miundombinu ya usafiri, mafuriko na msongamano wa magari.
Kwa msafiri ambaye anatarajia kuja Dar es salaam kwa siku ya kesho ni vyema ukazingatia aina ya mavazi ya kuvaa na muda wa kufika kwani nyakati za usiku hali inakuwa mbaya zaidi kwa wale wanaotumia usafiri wa umma.
Post A Comment: