Mashindano
ya shule za sekondari ya Copa Umisseta, yalizinduliwa Zanzibar kwa
shamrashamra mbalimbali za michezo na burudani katika uwanja wa Aman na
kuhudhuriwa na viongozi wa serikali,wadau wa michezo na wanafunzi wa
shule za sekondari na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud.
Mkuu
wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, alisema suala la michezo Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar inalipa kipaumbele kikubwa kwa kuwa inaamini kuwa
inayo faida nyingi baadhi yake ikiwa ni kujenga afya,kuleta
umoja,burudani na inazo fursa kubwa za ajira hususani kwa vijana na
aliipongeza kampuni ya Coca-Cola kwa kuwa mstari wa mbele kudhamini
mashindano haya.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Ayoub Mohamed Mahmod akipokea zawadi ya
mpira wa kufanyia mazoezi kutoka Coca-Cola baada ya hafla ya uzinduzi.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Maghribi, Ayoub Mohamed Mahmod (wa tatu kulia)
akikabidhi jezi na mpira kwa mwalimu Mussa Abdi Khamis wa shule ya
sekondari ya penae.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud, akipiga mpira kuashiria uzinduzi wa mashindano ya Copa UMISSETA.
Moja ya timu ikikaguliwa wakati wa uzinduzi huo.
Wananchi wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi.
Post A Comment: