Shahidi wa nne upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili mmiliki wa Shule ya Lucky Vicent, Innocent Mushi pamoja na makamu mkuu wa shule hiyo, Longino Nkana jana ameieleza Mahakama ya Wilaya ya Arusha kuwa gari lililobeba wanafunzi wa shule hiyo halikuwa na kibali cha kusafirisha wanafunzi.

Shahidi huyo, Allen Mwanri (48) ambaye ni ofisa mfawidhi wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) alisema gari hilo lilipewa leseni ya kusafirisha abiria kutoka wilayani Arusha kuelekea Mirerani Mei 16, 2016 na kiliisha Mei 15, 2017.

Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Desdery Kamugisha shahidi huyo aliieleza mahakama kwamba kwa mujibu wa kumbukumbu za ofisi, haijawahi kupokea maombi yoyote ya kubadilisha matumizi ya leseni ya gari hilo tangu kumalizika kwa leseni yake.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi leo  ambapo shahidi mwingine upande wa mashtaka atafika mahakamani hapo kuwasilisha utetezi wake.

Wanafunzi 32 wa shule hiyo, walimu wawili na dereva Mei 6, 2017 walifariki dunia kwa ajali ya basi la shule hiyo eneo la Rhotia, Karatu mkoani Arusha wakati wakielekea Karatu ambako watoto hao walipaswa kufanya mtihani wa kujipima uwezo na wale wa Shule ya Tumaini.

Wakati kesi hiyo ikiendelea baadhi ya wazazi ambao watoto wao walifariki katika ajali hiyo walikuwa nje ya mahakama hiyoa
Share To:

msumbanews

Post A Comment: